KUHUSU

Kuhusu Markaz Zaid nin Thaabit

Markaz Zayd bin Thābit – Online ni kituo cha elimu kinacholenga kufundisha Qur-aan Tukufu na lugha ya Kiarabu kwa njia sahihi, rahisi, na ya kisasa kupitia mfumo wa mtandaoni.Tunajitahidi kuwasaidia wanafunzi kujenga msingi imara wa kusoma na kuandika Kiarabu, sambamba na kujifunza Qur-aan kwa tajwid sahihi, ili kufikia kiwango bora cha uelewa na utendaji.

Dhamira Yetu
Kutoa elimu bora ya Qur-aan na Kiarabu kwa kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji, huku tukizingatia usahihi, ubora, na ufuatiliaji wa kila mwanafunzi.

Maono Yetu
InshaAllah, Kuwa kituo kinachoongoza katika utoaji wa elimu ya Qur-aan na lugha ya Kiarabu mtandaoni, na kuwafikia wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Tunachokiamini
Katika Markaz Zayd bin Thābit tunaamini kuwa:
~Kila mtu ana uwezo wa kujifunza Qur-aan kwa usahihi
~Elimu bora huanza na msingi sahihi
~Teknolojia inaweza kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa wote